Na Helena Magabe.
Vijana zaidi ya 1400 wa UVCCM kutoka Mikoa mbali mbali Nchini Tanzania bara pamoja na Visiwani walianza matembenzi ya zaidi ya kilometa 200 Oktoba 8 2024 kutoka Butiama Mkoani Mara kuelekea Mwanza lengo likiwa ni kuenzi kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Matembenzi hayo yamezinduliwa na mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi Wilaya Butiama ambapo alima sema lengo ni kuenzi kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere pamoja na kuelekea wiki ya Vijana na kilele cha mbio za mwenge na uhuru .
Alisema mwaka 1967 katika ofisi ya Kata ya CCM Mwitongo Baba wa Taifa alianzia hapo matembenzi hadi Jijini Mwanza hivyo walitumia fursa hiyo kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha Vijana kugombea na kuhamasisha Vijana wenzao kushiriki uchanguzi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 27.
Aidha alisema kilele cha matembenzi hayo ni oktoba 14 katika viwanja vya Ccm Kirumba na mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan na kuongeza kuwa iwe nvua au jua UVCCM itahakikiaha inailinda amani ya Tanzania.