Na Angela Sebastian- Bukoba
Wanachama wa Ushirika wa kuweka na kukopa wa Social responsibility (SR) women group uliopo mtaa wa forodhani kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,wimezindua mfuko wa kuweka na kukopesha wanachama wake ili kusaidiana na kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa chama hicho salaha Karugaba katika risala yao wakati wa uzinduzi wa mfuko huo uliofanyika ndani ya kata hiyo na kuhudhuriwa viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo mbunge wa viti maalum mkoa wa Kagera kupitia (Ng'os)Neema Lugangira ambaye alikuwa mgeni rasmi.
"Mfuko huu utasaidia wanachama kukopa kwa riba ndogo na kujiongezea kipato bila kuhangaika kwenda kukopa kwenye sehemu nyingine za mikopo zenye riba kubwa na za kuwaumiza hivyo,lengo la mfuko huu pia nikuhakikisha chama kinajiendesha chenyewe na kufikia malengo ya kuwa taasisi na kutoa ajira kwa vijana"alieleza Karugaba
Amesema walianza kwa kununua hisa moja kwa wiki ya shilingi 2,000 kila mmoja huku mwanachama akikopeshwa shl 200,000 tu na kurejesha baada ya miezi mitatu ambapo, kwa sasa kutokana na uaminifu wa wanachama hao kuona chombo hicho ni chao na pia ni kombozi wao wemeweza kukopa na kurejesha kwa wakati.
"Uaminifu huo wa wanachama umesababisha mtaji kukua na sasa tunaweza kununua hisa kuanzia shl 5000 na kuendelea kila mmoja na mwanachama anaweza kukopeshwa kati ya shl milioni moja hadi mbili,kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza ikiwemo mahitaji ya shule kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum kutokana na faida kidogo tunayoipata"ameeleza Karugaba
Aidha kutokana na faida wanayopata na kisha kugawana kidogo na jamii wameweza kuwachangia vifaa mbalimbali watoto wanne yatima walioshinda kwenda kidato kwanza mwaka huu, baada ya kushindwa kujiunga na masomo ambapo walipewa sare za shule,madaftari,kalamu na mabegi.
Misaada mengine ni wametoa unga wa uji kilo 100 na sukari kilo 25 katika shule ya msingi Bunena na Bakoba sekondari na bagi za madaftari kwa watoto wategemezi.
Naye katibu wa kikundi hicho Zamda Mkeku anasema uwepo kwa kikundi hicho imewasaidia kukuza kipato chao na kuepuka utegemezi ambapo mwanachama akipata shida ya dharula mfano kulipia karo za watoto,chakula,ujenzi wa makazì bora,kurejesha sehemu ya faida kwa jamii tegemezi na mahitaji mengine ya msingi anakopeshwa ambapo wameepukana na mikopo umiza.
Mkeku anasema kikundi hicho kilianza 2021 kikiwa na wanachama saba na sasa kina wanachama 200 baadhi yao wakiemo vijana na wanaume
Kwa upande wake Neema Lugangira ambaye ni mbunge viti maalum mkoa wa Kagera pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliwapongeza kwa wazo la kuanzisha ushirika huo ambao utawaletea maendeleo yenye tija na kuwakwamua na lindi la umaskini na kuondokana na utegemezi.