Fahamu Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Vifaa Vya Umeme wa Solar

GEORGE MARATO TV
0

Na Emmanuel Chibasa

Umeme wa solar ni aina ya umeme unaozalishwa kwa kutumia mionzi ya jua. Paneli za solar, ambazo hujulikana pia kama photovoltaic (PV) panels, zinakusanya mionzi ya jua na kuibadilisha kuwa umeme wa kutumia nyumbani, ofisini, au kwenye shughuli nyingine za kibiashara.

Mfumo wa umeme wa solar unajumuisha paneli za solar, battery za kuhifadhi umeme, na inverter ambazo hubadilisha umeme wa DC (Direct Current) kutoka kwenye paneli kuwa umeme wa AC (Alternating Current) unaotumika katika vifaa vya umeme vya kawaida.

Umeme wa solar unafaa kwa shughuli nyingi, hasa katika maeneo ambapo umeme wa gridi ya taifa haupo au unapatikana kwa ukawaida. Mfumo huu ni wa kuaminika na wa gharama nafuu, kwani unategemea chanzo cha nishati kisicho na mipaka—jua. Hivyo, umeme wa solar unafaa kwa matumizi mbalimbali kama vile mwanga wa nyumba, matumizi ya vifaa vya kielektroniki, na hata kwa biashara ndogo na mashamba.

Licha ya umeme wa solar kuwa nafuu na uhakika Kwa Matumizi Mbalimbali hasa Kwa Wananchi wa maeneo ya vijijini, Changamoto kubwa ni uelewa juu ya matumizi sahihi ya vifaa Toka Kwa wataalam Hali inayopelekea nishati hiyo Kutumiwa na watu Wachache 

Khamis Haule ni mkazi wa wilaya ya Musoma mkoani Mara mwenye familia ya watoto wanne na mfanya Biashara nataka anasema amekuwa akijitahidi kutafuta suluhisho tatizo la umeme nyumbani kwake na alijua kwamba umeme wa solar unaweza kuwa suluhisho bora.

Amesema ameshindwa kufanya mamuzi ya kunununua solar kutokana na kukosa  uelewa jinsi ya kuchagua vifaa sahihi na vinavyofaa katika shughuli mbalimbali tofauti na kupata mwanga kwenye nyumba yake kama anavyoona kwa watu wengine kutokana na kusikia baadhi ya watu wakilalamika vifaa kutokidhi Mahitaji kama walivyofikiri awali

Mbali na Khamis nimezungumza pia pia na Grace Matiku ambaye ni mama wa familia ili kupata kufahamu uelewa wake kuhusu matumizi ya umeme wa Solar  amesema kuwa binafsi anafahamu kuwa umeme wa solar unatumika majumbani kwa ajili ya kupata mwanga Kwa watu ambao hawana umeme lakini pia Kwa Wenye umeme wa tanesco kupunguza matumizi.

“ Mimi kwangu sijaweka solar lakini naona siku hizi watu wengi wananunua solar ili kusaidia mwanga katika taa za nje kwa ajili ya ulinzi lakini pia zinasaidia kupata mwanga na zile taa za barabarani, ila sijawahi kwenda dukani kujua zaidi juu ya matumizi zaidi ya kuona vifaa vyake vimepangwa na kuuzwa kwenye baadhi ya maduka” Amesema Grace.

Khamis na Grace ni miongoni mwa wananchi ambao pia wengi wao wamenunua vifaa vya solar bila kuwa na uelewa wa kutosha juu ya mambo gani wanapaswa kuzingatia kabla ya kufanya manunuzi ya vifaa au kutafuta wataalam ili waweze kuelimishwa zaidi.

Katika kusaidia kutatua changamoto hiyo nimezungumza Joachim Misana ambaye ni mtaalam wa solar na mwenye uzoefu  ili kufahamu ni mambo gani muhimu ya kuzingatia kabla ya kununua vifaa vya solar ikiwa ni pamoja na hatua muhimu za kuchagua paneli za solar na battery zinazofaa.

Amesema kabla ya kununua vifaa vya solar kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, biashara au kilimo kwanza mtu anahitaji kuelewa matumizi yake ya umeme kwa kuorodhesha vifaa vyote wanavyotumia na kiasi cha umeme vinavyotumia pamoja na kuonyesha jinsi ya kuhesabu matumizi yote kwa kutumia vigezo vya Watt na masaa ya matumizi huku akieleza hatua za kufuata katika matumizi yake

Hatua ya Kwanza  ameekezea jinsi ya kuchagua paneli za solar zinazofaa kwa kuzingatia ukubwa wa paneli ambapo amesema kuwa paneli kubwa zinakusanya mionzi ya jua kwa kiasi kikubwa na kwa muda mfupi zaidi na ukubwa na idadi ya paneli zinazohitajika zitategemea idadi na aina ya vifaa vya umeme vinavyotumika, muda wa matumizi, na kiwango cha mwangaza wa jua katika eneo.

Hatua ya Pili: Rashid alisisitiza mambo matatu muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua paneli za solar kwa kuangalia matumizi ya Umeme kwa kuangalia  ni vifaa gani vya umeme vinavyotumika na kiasi gani cha umeme vinavyotumia, Kufahamu ukubwa na uwezo wa battery unayohitaji pamoja na kuangalia uwezo wa Solar Panel kwa kuangalia ni za ukubwa gani (au idadi ya paneli) zitakazozalisha umeme wa kutosha kuchaji battery kwa haraka.

Hatua ya Tatu amefafanua kuwa ili mtu aweze kumudu vyema mtumumizi ya solar anapaswa kufahamu pia jinsi ya kupima kiasi cha umeme kinachotumika kwa kila kifaa kwa kutumia kipimo cha Watt (W). Kwa mfano, kwa taa yenye nguvu ya 24W inayotumika kwa masaa manne (4), alieleza jinsi ya kuhesabu umeme inayotumiwa kwa jumla, ambayo ilikuwa 96Wh kwa masaa manne.

Hatua ya nne ni kuwa na uelewa wa jinsi ya kupima uwezo wa battery kwa kutumia kipimo cha Amp Hours (Ah) na Voltage (V).Huku akitolea  mfano wa battery yenye uwezo wa 17Ah na voltage ya 12V, na jinsi ya kuhesabu umeme itakazotoa kwa kutumia formula ya Watt: 17Ah x 12V = 204Wh na kueleza  kwamba battery hii inaweza kuwasha taa yenye nguvu ya 24W kwa masaa 8.5.

Na hatua ya Tano alieleza na kusisitiza umuhimu wa kujua kiasi gani cha umeme solar panel yako inaweza kuzalisha kwa muda gani na kusema  kwamba  mtumiaji anapaswa kufahamu uwezo wa solar panel kupima kwa kutumia Watts (W) na masaa ya mionzi ya jua. Kwa mfano, paneli ya 10W inayopokea mionzi ya jua kwa masaa nane (8) itazalisha 68Wh na pia mtumiaj anahitaji kuhesabu ni paneli ngapi zitahitajika ili kufikia mahitaji yao ya umeme.

Joachim anatoa wito kwa watumiaji wanaotaka kununua vifaa vya solar kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, biashara na kilimo, kwanza kuwashirikisha wataalam ili waweze kujengewa uelewa wa matumizi lakini pia kupata ushauri wa kuchagua solar panel pamoja na betri zitakazoendana na mahitaji husika.

Pia ameongeza kuwa kuwaona wataalam kunasaidia kufahamishwa namna ya matumizi na utunzaji wake kuliko kwenda dukani kununua vifaa kabla ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamili kuhakikisha kwamba wanapata mfumo wa umeme wa solar utakaokidhi mahitaji yao ya umeme kwa ufanisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top