WADAU GEITA WAPONGEZA MIFUMO MIPYA YA MITIHANI YA TAIFA

GEORGE MARATO TV
0

Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Kadama, Mwalimu Leticia Pastory, amesema kuwa mabadiliko ya mfumo wa mitihani ya Taifa kwa shule za msingi yanatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa wanafunzi.

 Akizungumza wakati wa mahafali ya kumi na nne ya shule ya Msingi ya Kadama, Mwalimu Leticia alieleza kuwa mfumo mpya utaimarisha ubora wa elimu na kuwaandaa wanafunzi kwa zaidi ya ajira za kawaida, huku pia ukilenga kuwawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.

Aliongeza kuwa mfumo huo utawajengea wanafunzi uwezo wa kujitegemea, ubunifu, na ujasiriamali, vitu ambavyo ni muhimu sana katika mazingira ya sasa ya kiuchumi. 


"Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuboresha elimu ya msingi, na tunaamini yatasaidia sana kuandaa vijana wenye ujuzi wa maisha," alisema Mwalimu Leticia.

Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Mboje Kisusi, aliwasisitiza wazazi na walezi umuhimu wa kuwafundisha watoto wao maadili mema na kumjua Mungu, akiongeza kuwa elimu bora inapaswa kuendana na malezi ya kiadili.

Mahafali hayo yalihudhuriwa na wazazi, walezi, na wadau mbalimbali wa elimu, ambapo walipongeza juhudi za shule hiyo katika kutoa elimu bora na kumlea mtoto kiadili na kitaaluma.Huku wanafunzi 73 wakiwa wamehitimu.

mwisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top