Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera *Ndugu Faris Buruhani,* ameshiriki fainali ya mpira wa Miguu ya BASHUNGWA KARAGWE CUP 2024 ilitofanyika katika uwanja wa mpira wa Bashungwa mjini Kayanga Karagwe.
Fainaili hiyo ambayo imefanyika. Agosti 25-2024 imekuwa ya aina yake na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Karagwe na wilaya jirani, sambamba na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Ligi hiyo imetamatika kwa timu ya *Nyabiyonza FC kuibuka Mshindi* katika mashindano hayo kwa kunyakua
Kombe, *pesa taslimu 6,000,000/= (milioni sita)* na zawadi nyingine kutoka kwa kamati ya mashindano hayo.
Bashungwa Karagwe Cup 2024, ni mwendelezo wa mashindano ya mpira wa miguu yanayoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Karagwe *Mh. Innocent Bashungwa* kila mwaka, yenye lengo la kuwaleta vijana pamoja, kuibua vipaji vya vijana na pia kuwainua kiuchumi kupitia vipaji vyao.