Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuwa jeshi na Taifa linatambua ushindi na mafanikio makubwa yaliletwa na wanamichezo nchini hasa kwa timu za majeshi kwa kutumia jasho na damu katika kuliheshimisha taifa ndani na nje ya nchi.
Jenerali Mkunda ametoa kauli hiyo Septemba 26 mwaka huu 2025 katika viwanja vya Lugalo Goff Club jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kuwapongeza wanamichezo kutoka kwa jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania (Ngome) Jeshi la kujenga Taifa (JKT,),timu ya Wanawake wa JKT QUEENS na mwanariadha Alphonce Simbu.
Mkuu huyo wa mejeshi. katika sherehe hiyo,amesema jeshi limeandaa hafla hiyo kwa kutambua ushindi na mafanikio yaliyoletwa na wanamichezo katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Kwa hiyo ameipongeza timu ya Ngome kwa kutwaa ushindi wa jumla katika mashindano ya BAMMATA Zanzibar na kusema ushindi huo umeonesha thamani ya mshikamano na nidhamu miongini mwao.
"Timu ya Ngome imeweka alama na mfano mkubwa wa kuigwa na hivyo kuliletea heshima kubwa jeshi letu,vilevile nawapongeza wao JKT kwa kuwa mshindi wa pili kati ya kanda saba zilizoshiriki kwa ujumla Ngome na JKT wameliheshimisha jeshi sana jeshi letu"alisema Jenerali Mkunda.
Aidha mkuu huyo wa majeshi ameipongeza timu ya JKT gueens kwa kutwaa ubingwa wa mashindo ya mpira wa miguu wanawake 2025 CECAFA iliyofanyika Nairobi nchini Kenya.
Kuhusu ushindi wa mwanariadha Simbu,jenerali Mkunda amesema kuwa ushindi wa Simbu si fahari tu kwa jeshi la ulinzi la wananchi bali ni fahari kubwa kwa taifa kiujumla na kitendo cha ushindi huo Simbu ameweka mfano wa kuigwa kwa hadi tone la damu.
"Kipekee kabisa napenda nimpongeze staff sajenti Simbu,kwa kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Marathon ya kimataifa ya kilometa 42 yaliyofanyika Tokyo Japan septemba 15 mwaka huu 2025,huu ni ushindi mkubwa na ushindi wa kwanza katika historia ya riadha ya nchi yetu katika mashindano makubws kama haya"alisema Jenerali Mkunda na kuendelea.
"Na ushindi huu si tu ni fahari kwa jeshi letu bali na kufahari kubwa kwa taifa letu la Tanzania,staff sajanti Simbu ni mpambanaji mwenyekuweka viwango,lengo na kulipigania lengo hilo hadi anapofanikiwa,kwa kweli amewaka mfano wa kiigwa kwa tabia ya kijeshi ya moyo hadi tone la damu.....hongera sana staff sajenti Simbu kwa majeshi ya kulihemisha jeshi mkuu wetu"aliongeza.
Hata Jenerali Mkunda ame wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulitengeneza jeshi na kutekeleza majukumu yake kutuma kutuma michezo ambapo pia amesema mchango wa Rais Samia mkubwa na unaoleta matunda katika sekta ya jeshi.
Amesema Kuwa michezo ni nyenzo ya kuleta furaha umoja, afya, mshikamano, nidhamu pamoja na heshima katika jamii.
Jenerali Mkunda pia, ametoa rai kwa wananmichezo kuendelea kuchukua vikombe na medali mbalimbali wanazoshiriki ndani na nje ya nchi ili kuipaisha vyema bendera ya Taifa la Tanzania.
Kwa hiyo ametumia fursa hiyo kuagiza viongozi wote wa michezo jeshini kuendelea kufikia ushindi wa mashindano yotè yajayo.
Kwa Upande wake, Mkuu wa Opareaheni na mafunzo ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania, Meja jenerali Ibrahim Mhona amesema ushindi wa wanamichezo hao sio tu sifa katika jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania bali ni kulitangaza taifa kitaifa na kimataifa.
Pia, amesema kuwa mafanikio yanayonekana leo ni miongoni kwa maerekezo, uwezeshaji wa mkuu wa majeshi ambayo huchochea hali ya kujiamini kwa wanamichezo katika michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Aidha, Meja jenerali Ibrahim Mhona amempongeza jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa jeshi la kujenga taifa (JKT) kwa jitihada zake za kulea timu hizo hadi kupelekea kuibuka kidedea katika michuano mbalimbali.i.