NSSF watakiwa kufikia malengo, kushiriki uchaguzi

GEORGE MARATO TV
0


Na MASHAKA MHANDO,Tanga

BODI ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeigiza bodi ya wakurugenzi ya Mfuko huo, kuhakikisha wanatekeleza malengo waliyojiwekea ikiwemo kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao.

Akifungua mkutano wa 54 wa baraza kuu la wafanyakazi wa NSSF, Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini Mwamini Juma Malemi alitaka bodi iongeze ukuaji wa mfuko kwa kuongeza wanachana lakini pia kuongeza kasi ya makusanyo ya michango kutoka kwa wanachana.


"Ndugu wajumbe naomba nisisitize na kutoa maagizo sita, moja uadilifu na kupiga vita rushwa, wafanyakazi wawe waadilifu na watimize wajibu wao," alisema.

Pia aliagiza kuimarishwa kwa mifumo ya Tehama ili kuongeza makusanyo lakini pia isiweze kupotea kwa urahisi.

Aidha, bodi imeagiza menejmenti kuhakikisha wanalipa mafao kwa wakati na kuondoa manung'uniko ya awali ya wastaafu kuchelewa kulipa mafao yao licha ya wanachama kutimiza taratibu zote.

Mwenyekiti huyo wa bodi ya Wadhamini pia aliagiza wahakikishe wanaimarisha mfumo wa uchangiaji wa hiari kwa sekta binafsi wanachama wanajitokeza na kujiunga na mfuko.

"Mfumo wa uchangiaji wa hiari uimarushwe, elimu itolewe ili waweze kujiunga katika mfumo huo ambao ni muhimu na ni mzuri kwani utawawezesha wanachama kunufaika na michango yao wanayotoa," alisema.

Pia, agizo la mwisho alilolitoa Mwenyekiti huyo ameagiza bodi iendelee kufanyia kazi changamoto za kiutendaji zilizopo za kimfumo ili waweze kuzimaliza kwa haraka.

"Mwisho ndugu wajumbe tunawaomba mshiriki uchaguzi Mkuu ujao kwakuwa ni haki yenu lakini pia nyie ni vioo kwa Jamii hamasisheni watu wengine watumie haki yao ya kupiga kura," alisema.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Masha Mshomba alisema mfuko huo alisema mkutano huo wa baraza unajadili mpango wa mwaka wa mfuko na bajeti ya mwaka 2025-2026.

Alisema mapendelezo ya mpango wa bajeti ya mwaka 2025/26 ambapo kipindi Cha mwaka 2024/25 thamani ya Mfuko ilikuwa ni kiasi cha shilingi Trilioni 9.91 hadi kufikia Juni mwaka huu.

Alisema hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu,  thamani ya Mfuko ilikuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 9.6 na wana uhakika wakienda hivyo mwisho wa mwaka watafikia malengo.

Alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha mpango wa bajeti ni kiasi cha shilingi Trilioni 11.72 hadi kufikia Juni 2026.

Alisema kuwa ukilinganisha mpango wa saba wa bajeti unaoisha Juni 2026 walijiwekea  ukuaji wa mfuko kwa thamani ya shilingi Trilioni 11.54 wamefikia lengo kwa asilimia mbili.

Pia wamelipa mafao na gharama za uendeshaji na malengo yao kwa kiasi cha shilingi trilioni 2.99 katika mwaka ujao wa fedha.

Mkurugenzi mkuu alisema wamejipangia mwaka ujao wa fedha mapato ya uwekezaji ya  takribani shilingi bilion 765.32 na kwamba malipo ya mafao yatakuwa takribani shilingi za Kitanzania shilingi Trilioni 1.13 malipo hayo yatakuwa ni nyongeza ya asilimia 21 ukilinganisha na malipo wanayotarajia kufanya mwisho wa mwaka huu ya bilioni 932.

"Tunategemea gharama za uendeshaji ziende sambamba na viwango vilivyowekwa na wakaguzi wa sekta ya Hifadhi ya Jamii na wanatarajia watakuwa na asilimia 13.6 ya makusanyo yote ya jumla ya matumizi ya Mfuko,“ alisema.

Pia alisema taswira ya ukuaji wa mfuko alimpongeza Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini, wakurugenzi na watumishi wa mfuko huo kwa ukuaji wa mfuko kwa viwango hivyo vinaakisi juhudi walizofanya.

Pia wanampongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na juhudi zake ambazo zimechangia ufanisi wa mfuko kutokana na uwekezaji katika sekta binafsi kwa miaka hii minne.

Alisema Rais amechangia ongezeko la wanachama na kuongezeka kwa Pato la uwekezaji lakini pia mfuko huo imepiga hatua kubwa sana 

"Tunampongeza sana Mhe Rais kwa ambavyo amesaidia maboresho katika sekta binafsi lakini pia wanachama wamejiunga kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali," alisema.

Pia Mkurugenzi mkuu alisitiza uchangiaji wa hiari ambao ni kitu muhimu na wanavipa kipaumbele na wanataka watanzania wajitokeze kujiunga katika mpango huu ambao utawawezesha kupata kipato kitakachowasaidia katika maisha yao.

Kuhusu uchaguzi aliwataka wafanyakazi wa mfuko huo kuhakikisha wanashiriki katika uchaguzi huo kwa kuchagua viongozi ambao watalivusha Taifa la Tanzania.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top