Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga, leo Januari 25, 2025 amezindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Manyara.
Maadhimisho hayo yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani Babati mjini Mkoani Manyara yenye lengo la kutoa Elimu na msaada wa kisheria kwa wananchi, yanayoanza leo Januari 25 na kumalizika Februari 3, 2025 huku kaulimbiu ikiwa ni "Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo".
Aidha, RC Sendiga amewaasa na kuwakumbusha watumishi wa mahakama na wadau kutenda haki na usawa kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi yao ili waweze kutatua changamoto za Wananchi na kuleta tija.
Sambamba na hilo amewasihi Wananchi wajiepushe na wanasheria vishoka ambao wamekuwa wakiwadanganya wananchi wanaohitaji huduma za kisheria
Uwajibikaji rafiki wa maendeleo 🇹🇿




