Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati Doto Biteko anatarajia kuwa mgeni Rasmi katika tamasha kubwa la ijuka Omuka linalolenga kuwakutanisha wazawa wa mkoa wa Kagera,wanaoishi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujadili fursa za uwekezaji zilizoko mkoani humo.
Mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa ambaye ni mwanzilishi wa tamasha hilo akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake amesema kuwa, tamasha hilo litaanza tarehe 18 Hadi 26 Desemba na kujumuisha maonyesho makubwa ya kibiashara na kutambulisha utamaduni halisi wa wakazi wa mkoa huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko.
Amesema ufunguzi wa tamasha hilo utafanyika tarehe 19 Desemba ambapo wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watajadili fursa za uwekezaji katika sekta za ujenzi wa viwanda na utalii zinazopatikana mkoani humo na kuangalia namna mkoa unavyoweza kurudi katika uchumi wake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
"Mwaka Jana tulifanya ijuka omuka na mpaka sasa Kuna mafanikio japo haikuwa ya watu wengi ,mwaka huu tunaangalia namna ya kufanya maonyesho makubwa yenye vionjo mbalimbali kama kukutanisha wadau wakubwa wa ndani na nje ya mkoa na kujadili kwa upana na kuangalia namna ya kuinua mkoa kiuchumi kwa namna moja au nyingine "anasema Mwassa.
Aidha anasema tamasha hilo litakuwa na burudani Nyingi kutoka kwa wasaniii pamoja na utamaduni wa mapishi ya vyakula vya asili ambavyo vimesahaurika kama ukumbusho wa utamaduni halisi wa wakazi wa mkoa wa Kagera.
Ametaja matukio manne ambayo yatafanyika katika tamasha hilo kwa siku tofautitofauti kuwa ni dua ya kuombea mkoa,Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ambayo itafanyika Desemba18 ,tarehe 19 ni kongamano la wafanyabiashara na tamasha la utamaduni wa mtu wa Kagera.
Pia Desemba 20 yatafanyika mashindano ya pikipiki,maonesho ya mavazi na muziki wa pwani,tarehe 21 mashindano ya mpira wa miguu kati ya Kagera sugar na Simba aidha wasaniii mbalimbali wa kizazi kipya watatumbuiza, pia maonesho ya biashara yanaendele hadi Desemba 26 mwaka huu.

.jpg)

