Brig. Jen. PE Ngata, Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Comoro ametembelea Mradi wa Kilimo (CRDE) MITSAMIHOULI. Akiwa kituoni hapo, Brig. Jen. Ngata ameonesha nia ya kushirikiana na kituo hicho katika kuimarisha uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Kituo cha CRDE Mitsamihouli kinajihusisha na utafiti wa mazao ya mizizi, na Ufugaji.
Sambamba na ratiba hiyo, Brig. Jen. Ngata alipata nafasi ya kutembelea kijiji cha Hantsindzi Mboimkuu na kukagua mradi wa ujenzi wa Barabara ya kijijini ambayo Kampuni ya SUMA JKT inaendelea na majadiliano ya zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mradi huo unatarajiwa kuwa kazi ya kwanza kutekeleza na Kampuni ya SUMA JKT nchini Comoro.
Mapema siku hiyo, Brig. Jen. Ngatta na Ujumbe wake walitembelea Kampuni ya Ujenzi ya SCPMC inayoendelea na ujenzi wa majengo ya Kiutawala katika Uwanja wa Mpira Mitsamihouli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Ben Daroueche Nagib alionesha tayari wa kuanzisha ushirikiano na Kampuni ya SUMA JKT ili kushirikiana kutekekeza miradi ya ujenzi.
![]() |