Na Robinson Wangaso-Musoma.
Wadau wa maendeleo mkoani Mara wameshauri tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kutofautisha Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2025 na Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu 2024.
Akitoa ushauri huo, Katekista Peter Benard kutoka kanisa LA Roman Catholic amesema elimu ya uboreshaji wa daftari la kudumu inahutajika ili kutofautisha Matumizi daftari hilo katika Uchaguzi mkuu Na ule wa Serikali za mitaa.
Akifungua mkutano wa wadau mkoani Mara Mwenyekiti tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Jaji Jacobs M. Mwambegele amewaasa wadau kuhamasisha wananchi kujitokeza Kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Jaji Mwambegele ameyasema hayo leo Agosti 25, 2024 katika Mkutano wa Tume huru ya taifa ya Uchaguzi kuhusu uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura uliyofanyika mkoani Mara katika ukumbi wa uwekezaji katika ofisi za mkuu wa mkoa.
Amesema zoezi la uboreshaji litawahusu wananachi wanahitaji kuboresha au kurekebisha taarifa zao kama kuhama kituo cha kupigia kura, wale wote waliopoteza vitambulisho na wenye changamoto za majina.
![]() |
Aidha amesema zoezi hilo haliwahusu wapiga kura ambao kadi zao hazina tatizo hivyo kadi za zamani za wapiga kura zitaendelea kutumika.
Kaulimbiu ya zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura ni "Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora."
Akiwasilisha mada katika mkutano huo mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani, amebainisha Makundi yatakayohusika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kuwa ni pamoja na kuandikisha wapiga kura wapya, wapiga kura waliohama vituo, wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura na kuondoa waipga kura waliopoteza sifa za kuwa kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali.
Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa kuwa wadau mbalimbali zikiwemo vyombo vya habari, vyama vya siasa, viongozi wa Dini mbalimbali wanao mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kuboresha daftari la kuduma la wapiga kura.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Mara litafanyika kati ya Septemba 4, 2024 mpaka Septemba 10, 2024.