Amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Dr Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itatumia kila uwezo katika kuimarisha jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania.
Rais Samia ametoa kauli hiyo Agosti 28-2024 jijini Dar es Salaam,wakati akikabidhi mabasi ya kisasa na ndege kwa ajili ya mafunzo kwa marubani kwa mkuu wa majeshi ya ulinzi jenerali JACOBO JOHN MKUNDA.
Rais Samia pamoja na kulipongeza JWTZ kwa kazi kubwa inayofanya katika mipaka ya Tanzania, amesema lazima serikali iendelea kuliimarisha kwa kulipatia zana na vifaa vya kisasa ili liwe tayari kukabiliana na matishio yoyote ya kiusalama.
Kwa sababu hiyo Rais Samia, amesema pamoja na serikali kuendelea kuimarisha hilo,amewataka Watanzania kutambua kuwa suala la ulinzi wa mipaka ni jukumu la kila Mtanzania.
Kwa upande wake waziri wa ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Dtk Stergomena Tax,amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake imara ambao umeimarisha diplomasia ya ulinzi na mataifa mengine.
Kwa upande wake mkuu wa majeshi ya ulinzi jenerali JACOBO JOHN MKUNDA,ameendelea kumpongeza Rais Samia, kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuimarisha jeshi hilo kwa kulipatia mitambo, zana na vifaa vya kisasa.
Hafla hiyo imeudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,maafisa na askari wa ngazi mbalimbali wa jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania.