MTIA nia nafasi ya Ubunge katika jimbo la Kwimba Cosmas Bulala amelalamikiwa kwa kuanza kampeni kabla ya muda jimboni humo, jambo ambalo limedaiwa linakinzana na maelekezo ya chama hicho.
Malalamiko hayo yaliibuliawa jana Juni 9, 2025 na baadhi ya wana CCM wilayani humo waliofika Jijinil Mwanza katika ofisi za chombo hiki ili kupaza sauti zao kwa lengo la kushinikiza mamlaka za juu kumchukulia hatua kali Bulala.
"Haiwezekani maagizo yalikwishatolewa na ngazi za juu kuwa ni marufuku kuanza kampeni kabla ya muda, na woke, tunasubiri lakini yeye tayari ameshaanza, nadhani hatua zichukuliwe dhidi yake maana hizo ni vurugu hazikubariki" aliapa mmoja wao.
Taarifa zinasema jana Juni 9, 2025 majira ya 14:00 mchana huko Hungumalwa kwenye kituo cha mafuta cha MDR alionekana mtu wa karibu na Bulala akiwawalipia bidaboda petroli ya shilingi 4,000/- waliovalia reflector jacket zilizochapishwa jina lamtia nia huyo, "Bulala".
Aidha taarifa zinaongeza kuwa, mbali na tukio hilo, lingine ni lile la siku kumi zilizopita ambapo Bulala alionekana akiwagawia pesa baadhi ya wajumbe jimboni humo kiasi cha 40,000/- katika maeneo kadhaa ya Jimbo hilo jambo ambalo limetafsiriwa kama uvunjaji wa kanuni.
"Mimi nilishuhudia pesa zikitokewa kwa baadhi ya wajumbe, huku wajumbe wakiombwa kumchagua Bulala pindi muda utakapowadia, nilijuuliza mambo mengi, huyu anayetanguliza pesa tena kabla ya muda akipata anachokitafuta atawakumbuka wananchi kweli?" alihoji mwingine.
Gmtv ilimtafuta Bulala kwa simu jana ili kupata ufafanuzi juu ya lawama hizo na kuonyesha kutotambua malamiko hayo Kwa alichosema yuko Jijini Dar es Salaam akiendelea na kazi zake.
"Nani analalamika? wanalalamika nini? Wamelalamika wapi? mimi sina mtu huko,sijafanya hayo mimi niko Dar es Salaam kaka na siwezi kufanya mambo hayo" alihoji na kusisitiza Bulala.
Alipotafutwa kwa simu Katibu wa CCM wilayani Kwimba Aghata Lubuva ili kuzungumzia sakata hili akadai ana taarifa ya suala hilo kwa madai kuwa lilimsikitisha sana tukio hilo akaahidi kiongozi wake Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Omary Mtuwa, kwa maelekezo.
"Nilikuwa sifahamu, lakini leo (jana) nimeona mtandaoni imerushwa ndio nimeipata vizuri, baada ya kuwaona bodaboda wamevalia reflector za jina lake, ikabidi nimpigie Bulala nikamwambia kuwa wanaomwambia kufanya hivyo wanamharibia" Aghata alisononeka.
"Kwa suala hilo itabidi nimtàarifu na Boss wangu Katibu wa Mkoa ili anipe maelekezo ili nisije nikakurupuka mambo yakawa tofauti maana na mimi bado ni mgeni katika Wilaya hii" alisema Aghata.
Alipotafutwa jana ofisini kwake, Mtuwa ambaye ndiye Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akadai ameona suala hilo mtandaoni, akadai anasubiri taarifa rasmi Kwa maandishi ili ofisi yake iweze kuchukua hatua.
"Kule wilayani kuna kamati ya maadili, kuna kamati ya siasa, hivyo mimi huku ni juu sana, haitafaa nikianza kulifanyia kazi kabla ya hatua hizo, lakini pia likiletwa kwa maandishi tutalifanyia kazi" Mtuwa alifafanua
Hata hivyo leo Juni 10, 2025 chombo hiki kilimtafuta Kamanda wa TAKUKURU mkoani hapa Mhandisi Abnery Manga ofisini kwake ili kujua hatua zinazochukuliwa na Taasisi hiyo dhidi ya Bulala lakini alikuwa nje ya ofisi ndipo mmoja wa maafisa wake akaahidi kuliahughulikia.
"Ahsante kwa taarifa nakuahidi litashughulikiwa, na mara nyingine inapotokea jambo kama hilo wawe wanatoa taarifa kwenye ofisi zetu za huko iwe rahisi kufanyiwa kazi 'on the sport' alidokeza Afisa huyo.